Miwati ni miti ya jenasi Acacia katika familia Fabaceae iliyo na majani yenye sehemu nyingi, lakini vikonyo vya majani vya spishi nyingi vimekuwa vipana na vimebadili majani menyewe. Zamani jenasi hii ilikuwa na spishi takriban 1300 lakini wanasayansi wameigawanya kwenye jenasi tano sasa: Acacia, Vachellia, Senegalia, Acaciella na Mariosousa[1]. Spishi za Acacia zinatofautiana na zile za jenasi Vachellia, Senegalia na Acaciella kwa ukosa wa miiba (ghairi ya muwati kangaruu). Hazina mastipula (majani mawili madogo chini ya jani kuu) kama spishi za Mariosousa. Kwa asili miti hii inatokea Australia lakini imewasilishwa katika mabara mengine.
Miwati ni miti ya jenasi Acacia katika familia Fabaceae iliyo na majani yenye sehemu nyingi, lakini vikonyo vya majani vya spishi nyingi vimekuwa vipana na vimebadili majani menyewe. Zamani jenasi hii ilikuwa na spishi takriban 1300 lakini wanasayansi wameigawanya kwenye jenasi tano sasa: Acacia, Vachellia, Senegalia, Acaciella na Mariosousa. Spishi za Acacia zinatofautiana na zile za jenasi Vachellia, Senegalia na Acaciella kwa ukosa wa miiba (ghairi ya muwati kangaruu). Hazina mastipula (majani mawili madogo chini ya jani kuu) kama spishi za Mariosousa. Kwa asili miti hii inatokea Australia lakini imewasilishwa katika mabara mengine.