Reptilia (kutoka Kilatini "reptilis" mwenye kutambaa; pia: mtambaazi, mtambaachi, mnyama mtambaaji[1]) ni kundi la wanyama wenye damu baridi, ngozi ya magamba badala ya nywele au manyoya wakipumua kwa mapafu. Siku hizi wataalamu hupendelea jina Sauropsida.
Wanazaa kwa njia ya mayai; wengine wanatega mayai na wadogo wanatoka nje bila ngazi ya kiluwiluwi au kwa spishi kadhaa mayai yanaiva ndani ya tumbo la mama na wadogo wanazaliwa hai.
Kibiolojia ni ngeli ya vertebrata. Jina limetokana na maumbile yao maana wanatambaa na tumbo juu ya ardhi; ama kwa miguu mifupi kama mijusi au bila miguu kama nyoka.
Dinosauria wa kale walikuwa reptilia wakubwa sana walikwisha miaka milioni 65 iliyopita. Kufuatana na vumbuzi za hivi karibuni ndege hufikiriwa kuwa na nasaba na dinosauri (kutoka kwa nusuoda ya Theropoda).
Joka wa Komodo ni mjusi mkubwa kabisa
Hata ndege ni reptilia!
Reptilia (kutoka Kilatini "reptilis" mwenye kutambaa; pia: mtambaazi, mtambaachi, mnyama mtambaaji) ni kundi la wanyama wenye damu baridi, ngozi ya magamba badala ya nywele au manyoya wakipumua kwa mapafu. Siku hizi wataalamu hupendelea jina Sauropsida.