dcsimg

Kunguru ( Swahili )

provided by wikipedia emerging languages

Kunguru ni ndege wakubwa kiasi wa familia Corvidae. Spishi nyingine huitwa vinubi. Wanatokea mabara yote isipokuwa Antakitiki. Spishi nyingi ni nyeusi au nyeusi pamoja na rangi ya nyeupe, kijivu au kahawa; nyingine zina rangi mbalimbali kama buluu, pinki n.k. Hula nusra kila kitu: wanyama na ndege wadogo, wadudu, mizoga, matunda, nafaka n.k. Hulijenga tago lao kwa vijiti juu ya mti au jabali. Spishi nyingine huyajenga matago kwa makundi. Jike huyataga mayai 3-10.

Kunguru na binadamu

Baadhi ya kunguru huonwa kuwa ni waharibifu na tunajua kwamba kunguru mkubwa kaskazi (Corvus corax), kunguru mkubwa wa Australia (Corvus coronoides) na kunguru mlamizoga (Corvus corone) wanaweza kuua wanakondoo dhaifu. Lakini mara nyingi hula mizoga iliyouawa karibuni kwa namna nyingine, ugonjwa k.m. Wengine wanaweza kuiga sauti ya binadamu, lakini hawawezi kuongea kama kasuku. Kunguru waliofundishwa kuongea, huonwa kama sehemu muhimu ya Asia ya Mashariki, kwa sababu kunguru huonwa kama alama ya bahati. Baadhi ya watu wanafuga kunguru kama wanyama wa nyumbani. Japo binadamu hawawezi kuwatambua kunguru, kunguru wanaweza kuwatambua watu na kuelewa kwamba hawa ni watu wabaya au la.

Kwa tamaduni nyingi za kienyeji za kaskazi ya mbali sana kunguru, spishi kubwa hasa, wamekuchwa kama viumbe vya kirobo au miungu. Katika Afrika Waxhosa wa Afrika Kusini waliwachukulia kunguru kuwa ni ndege wa Mungu. Hadithi ya kixhosa kuhusu shujaa aitwaye Gxam inasimulia kwamba kunguru walirudishia shujaa aliyefanywa upofu uwezo wake wa kuona. Hadithi nyingine ya Wasara wa Chadi na Sudani inasimulia kwamba Mungu mkuu, Wantu Su, alimpa mpwa wake wa kiume Wantu ngoma iliyokuwa ndani yake na mifano ya kila kitu kilichokuwamo mbinguni. Wantu alitarajiwa kuwapatia binadamu vitu hivi, lakini alikuwa akishuka kamba iliyounga mbingu na dunia, kunguru alipiga ngoma. Ngoma akaanguka duniani, akavunjika na akatawanya wanyama, samaki na mimea duniani kote.

Uwindaji

Huko Marekani kunguru huwindwa kwa kibali cha serikali. Isipokuwa kwanzia Agosti mpaka Machi, msimu wa uwindaji kunguru sababu huwa wengi na hapo watu huruhusiwa kuwinda kunguru. Huko Uingereza ni marufuku mpaka pale mtu atakapopewa kibali.

Tabia

Kunguru anamaamuzi ya haraka sana, na anamacho yenye uwezo mkubwa wa kuona, pia kunguru anaonekana kuwa na ujasiri mkubwa hamwogopi binadam wa kike (mwanamke)

Milio

Kunguru hutoa milio mbalimbali. Suala kwamba kuna mawasiliano ya kunguru ni aina ya lugha ni mjadala mkubwa mpaka leo. Kunguru pia wamejifunza kuitika milio ya wanyama wengine na tabia hii hubadilika kwa misimu kadhaa. Milio ya kunguru ni tata na migumu kuelewa, na milio yao hutofautiana kwa spishi tofauti na hasa ugumu wa kujifunza milio huja pale ambapo inafahamika kuwa kunguru wanauwezo wa kusikia sauti ndogo sana ambazo binadamu hawezi kuzisikia.

Akili

 src=
Kunguru aina Hooded Crow ya akitafuta chakula baada ya kutoboa mfuko

Kama kundi, kunguru wameonekana kuwa na akili sana na majaribio mbalimbali yamethibitisha hili. Kunguru wamepata alama za juu sana kwenye tafiti za awali. Kunguru wa huko Israeli wamejifunza kutumia vipande vya mkate kama chombo cha kuvulia samaki. Spishi moja, New Caledonian Crow, wamefanyiwa tafiti sana kutokana na uwezo wao wa kutengeneza zana za matumizi ya kila siku. [1]. Ujuzi mwingine ni ule wa kuangusha mbegu ngumu kwenye barabara inayopitisha magari makubwa ili yapasue, na kisha kusubiri taa za barabarani kuruhusu watu wapitie watawanye mbegu hizo. Na tafiti hivi karibuni zinaonesha kuwa kunguru wana uwezo wa nyuso za watu.

Virusi

Kunguru wa Amerika wanaathirika sana na virusi vya Naili Magharibi ugonjwa ulioanza hivi punde tu huko Amerika kunguru hufa ndani ya wiki moja tu tangu waupate ugonjwa huu na wachache sana hufanikiwa kupona. Kunguru wa huko huathirika sana na, kiasi cha kwamba kifo chao sasa kinaonesha athari ya virusi hao kwenye maeneo yao.

Uainishaji

Tangu miaka mingi wataalamu hawakubali kuhusu undugu wa familia Corvidae na jamaa yake. Mwishowe ilionekana kwamba kunguru wametokana na wahenga wa kiaustralasia na walitawanyika duniani kote. Majamaa yao ya karibu sana ni ndege wa peponi (birds of paradise), mbwigu na Australian mudnesters.

Kumbukumbu ya visukuku vya kunguru (mifupa yao) inaonyesha kwamba walikuwa wengi sana Ulaya lakini husiano baina ya kunguru wa kabla ya historia hazieleweki vizuri. Kunguru wa makubwa ya jackdaw, kunguru rangi-mbili na kunguru domo-nene wanaonekana kuwa walikuwepo tangu zamani sana. Kunguru waliwindwa na binadamu hadi enzi ya chuma, kitu ambacho kinaonyesha mabadiliko ya spishi za kisasa. Kunguru wa Marekani hawana historia sahihi inayoaminika. Chakushangaza spishi nyingi zimekwisha hivi sasa baada ya uvamizi wa binadamu, katika visiwa kama Nyuzilandi, Hawaii na Grinlandi hasa.

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Spishi za kabla ya historia

  • Corvus antecorax (Mwisho wa Pliocene – mwisho wa Pleistocene ya Ulaya)
  • Corvus antipodum (New Zealand Raven)
    • Corvus antipodum antipodum (North Island Raven) imekwisha sasa
    • Corvus antipodum pycrafti (South Island Raven) imekwisha sasa
  • Corvus betfianus
  • Corvus fossilis
  • Corvus galushai (Mwisho wa Miocene ya Big Sandy, Wickieup, MMA)
  • Corvus hungaricus
  • Corvus impluviatus ( High-billed Crow) imekwisha sasa
  • Corvus larteti (Mwisho wa Miocene ya Ufaransa)
  • Corvus moravicus
  • Corvus moriorum (Chatham Islands Raven) imekwisha sasa
  • Corvus neomexicanus (Mwisho wa Pleistocene ya Dry Cave, MMA)
  • Corvus praecorax
  • Corvus pliocaenus (Mwisho wa Pliocene – mwanza wa Pleistocene ya Ulaya ya Magharibi-kusini)
  • Corvus pumilis (Puerto Rican Crow) – labda nususpishi ya C.nasicus/palmarum
  • Corvus simionescui
  • Corvus viriosus (Robust Crow) imekwisha sasa
  • Pica mourerae (Mwisho wa Pliocene – mwanzo wa Pleistocene ya Mallorca)

Picha

license
cc-by-sa-3.0
copyright
Waandishi wa Wikipedia na wahariri

Kunguru: Brief Summary ( Swahili )

provided by wikipedia emerging languages

Kunguru ni ndege wakubwa kiasi wa familia Corvidae. Spishi nyingine huitwa vinubi. Wanatokea mabara yote isipokuwa Antakitiki. Spishi nyingi ni nyeusi au nyeusi pamoja na rangi ya nyeupe, kijivu au kahawa; nyingine zina rangi mbalimbali kama buluu, pinki n.k. Hula nusra kila kitu: wanyama na ndege wadogo, wadudu, mizoga, matunda, nafaka n.k. Hulijenga tago lao kwa vijiti juu ya mti au jabali. Spishi nyingine huyajenga matago kwa makundi. Jike huyataga mayai 3-10.

license
cc-by-sa-3.0
copyright
Waandishi wa Wikipedia na wahariri